Huwezi kusikiliza tena

Nguo za ndani za mitumba zinauzwa Uganda

Nguo kuukuu ni maarufu katika nchi zinazoendelea, yakiwemo mataifa ya Afrika. Kati ya nchi hizo ni Uganda, ambako wengi wanaweza kumudu bei ya mavazi hayo kuukuu.

Mara nyingi, nguo hizo ambazo pia huitwa mitumba au chagua eneo la maziwa makuu ni kutoka Ulaya, Korea ya Kusini na Marekani, na huwa ni za hali ya juu, licha ya kuuzwa kwa bei rahisi.

Lakini kabla ya kufika Kampala, tazama nguo hizo huwafikia vipi wateja. Nguo hizo zinapofika Kampala, biashara huwa ni kubwa mno, kiasi cha kuwavutia hata wafanyabiashara wa mataifa jirani ya Afrika Mashariki.

Siraj Kalyango ana maelezo zaidi.