Jamii ya Wamakonde kupewa uraia Kenya

Image caption jamii za kenya

Maelfu ya watu wa jamii ya Wamakonde wanapewa uraia wa Kenya kwa mara ya kwanza.

Kabila la Makonde linaloishi pwani ya Kenya walihama kutoka Msumbiji enzi za ukoloni kuja Kenya na kufanya kazi katika mashamba ya miwa.

Watakaposajiliwa, Jamii hiyo ya Wamakonde elfu tatu watapewa vitambulisho na kuwa kabila la 43 nchini Kenya.

Kushindwa kwao kujitambulisha kunamaanisha kwamba kwa miongo kadhaa wameshindwa kujisajili katika shule ama hata kutafuta kazi.