Wapiganaji wa IS wauteka mji nchini Iraq

Image caption Wapiganaji wa Islamic state wameuteka mji wa Ali Baghdad nchini Iraq

Marekani imethibitisha kuwa wanamgambo wa Islamic State wameuteka mji wa Ali Baghdadi ulio mashariki mwa Iraq karibu na kituo cha jeshi la Marekani.

Msemaji wa makao makuu ya jeshi la Marekani (John Kirby) alisema kuwa ni mara ya kwanza kwa miezi kadhaa ambapo wanamgambo wa islamic state wameliteka eneo jipya.

Mji wa Al Baghadad ulio kwenye mkoa wa Anbar uko umbali wa chini ya kilomita 10 kutoka kituo cha jeshi la wanahewa 300 wa Marekani wanaowapa mafunzo wanajeshi wa Iraq.

Mapema wanajeshi wa Iraq walikabiliana na kile kilichoonekana kuwa shambulizi la kujitolea muhanga dhidi ya kituo hicho.