Amkodishia mkewe mume wa 'kumhudumia'

Image caption mwanamume mmoja nchini kenya ameshtakiwa kwa kumshambulia mkewe baada ya kumtaka alale na mtu aliyemkodisha

Mtu mmoja katika mahakama ya Kwale nchini Kenya ameshtakiwa kwa kumkata pua na mkono mkewe ambaye anamshuku kwa kufanya uasherati.

Kulingana na gazeti la the Nairobian nchini Kenya,Chirope Mwaruwa anadaiwa kumkodisha mwanamume ili kulala na mkewe mjamzito akidai kwamba ana matatizo.

Alishtakiwa kwa kumshambulia mkewe Sada Dzea katika kijiji cha Mukundi taarafa ya Mangawani ,kaunti ya Kwale.

Kulingana na upande wa mashtaka Dzea mara ya kwanza alimkataa mtu aliyekodishwa na mumewe wafanye naye tendo la ngono akiwa mjamzito.

Baada ya Dzea kukataa mumuwe alianza kumshtumu kwa kufanya uzinzi huku akitaka kumvua nguo kwa lengo la kutafuta ushahidi.

Na alipokasirishwa na shtuma hizo Dzea alidaiwa kumtembelea mtu huyo aliyekodishwa na mumewe ili afanye naye tendo la ngono kwa lengo la kumfurahisha mumewe.

lakini kabla ya yeye kufika kwa mawanmume huyo mumewe mwenye wivu mwingi alidaiwa kumvamia na kuanza kumshambulia.