B Haram lashambulia mji wa Gombe Nigeria

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Boko Haram lashambulia mji wa Gombe nchini Nigeria

Kundi la wapiganaji wa Nigeria, Boko Haram, limeshambulia mji mkuu wa jimbo la Gombe, kaskazini-mashariki mwa Nigeria.

Watu walioutoroka mji wa Gombe, walieleza kuwa jeshi linapambana vikali na wapiganaji hao, na kwamba ndege piya zimetumiwa.

Boko Haram waliingia leo asubuhi katika vitongoji vya Gombe, baada ya kushambulia mji jirani uitwao Dadin Kowa.

Wapiganaji hao wamewahi kushambulia vitongoji vya mji wa Gombe, lakini hawakupata kujaribu kuuteka mji wenyewe.

Nigeria ilitarajiwa kufanya uchaguzi mkuu leo, lakini umeahirishwa kwa majuma sita, kwa sababu ya wasiwasi kuhusu usalama.