Waliokula fedha za ebola kusakwa S Leone

Haki miliki ya picha AFP
Image caption S Leone

Serikali ya Siera Leone inasema kuwa inatilia maanani ripoti maalum iliyogundua kuwa takriban dola milioni 14 zilizokuwa zitumike kupambana na ugonjwa wa ebola hazijulikani zilipo.

Msemaji wa serikali (Abdulai Bayraytay) aliiambia BBC kuwa yeyote ambaye atapatikana kuhusika kwenye ufisadi huo atakabiliwa na mkono wa sheria.

Mhasibu mkuu nchini humo ameshtumu wizara ya afya na idara inayohusika na ugonjwa wa ebola kwa kile alichokitaja kuwa ukiukaji wa sheria.