Arsenal yatinga robo fainali FA

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mchezaji wa Arsenal Olivier Giroud akifunga mojawapo ya magoli yake, ambapo Arsenal iliifunga Middlesbrough 2-0

Mabingwa watetezi wa Kombe la FA, Arsenal imefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali na kukomesha safari ya Middlesbrough ya kuwania taji hilo baada ya kuirarua mabao 2-0.

Magoli ya Arsenal yalifungwa na mchezaji wake Olivier Giroud.

Arsenal, ambayo ilimaliza ukame wa mataji uliodumu kwa miaka tisa kwa kushinda kombe la FA msimu uliopita, inaingia katika timu nane zitakazochuana hatua ya robo fainali ikiwa miongoni mwa timu tano za ligi kuu, mojawapo ni Liverpool iliyokwisha kata tiketi ya kucheza hatua ya robo fainali.

Katika michezo mingine iliyochezwa jana Jumapili, Bradford imeigaragaza Sunderland kwa kichapo cha mabao 2-0, huku Aston Villa ikiibwaga Leicester magoli 2-1.