Misri yataka UN kuishambulia ISIS Libya

Haki miliki ya picha AP
Image caption Rais Abdel Fattah el-Sisi wa Misri akiwafariji wakuu wa Kanisa la Coptic

Rais wa misri Abdel Fatah Al-Sisi ameutaka umoja wa mataifa kuidhinisha hatua za kijeshi za kimataifa dhidi ya kundi la Islamic State nchini Libya.

Akizunguma na kituo kimoja cha radio cha Ufaransa ( Europe One) rais Sisi alisema kuwa watu nchini Libya wanataka hatua kali kuchukuliwa ili kuleta usalama na udhabiti nchini mwao.

Al sisi alisema ''Hatutawaruhusu watoto wetu wachinjwe ovyo na hawa magaidi.''

Wito wa rais Sisi unakuja siku moja baada ya ndege za kivita za Misri kushambulia ngome za Islamic State kulipiza kisasi kuuawa kwa wamisri wa dhehebu la Coptic nchini Libya siku ya Jumamosi.

Hapo jana , Taarifa kutoka Misri zilisema kuwa, ndege za kijeshi ziliwashambulia wapiganaji wa jihadi nchini Libya kwa mabomu, baada ya kutolewa kwa mkanda wa video ulioonyesha wakristo wa Misri wa madhehebu ya Coptic

Image caption Misri yataka UN kuingilia kati Libya kuzuia kuenea kwa ISIS

wakikatwa shingo.

Jeshi la Misri lilisema kuwa lililenga kambi za Islamic State, kituo cha mafunzo na maghala ya silaha, katika shambulizi hilo la mapema leo alfajiri.

Walioshuhudia wanasema kuwa, mji wa Derna ulioko mashariki mwa Libya na ambao umetekwa na wapiganaji wa jihadi ndio ulioshambuliwa vibaya.

Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi, alisema kuwa mashambulio hayo ya angani ni jibu kwa wapiganaji hao ambao walitoa mikanda hiyo ya video hapo jana jumapili ilionyesha waumini kumi kati ya 21 waliotekwa nyara wakichinjwa.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ndege za kijeshi baada ya kutekeleza mashambulizi Libya

Waumini hao wa madhehebu ya Coptic walikuwa wametekwa nyara majuma kadha yaliyopita.

Jeshi la Misri lilitoa taarifa kwa vyombo vya habari ikisema kuwa raia wa taifa hilo walioko mbali ama karibu, wanafaa kuelewa kuwa wanajeshi la taifa linalowalinda kokote waliko.

Mamlaka ya Kiislam inayoongoza nchini Misri,-- Al Azhar -- imeshutumu mauaji hayo na kuyaita ni ya "kinyama". Maelfu ya Wamisri wamekuwa wakivuka mpaka kwenda kutafuta kazi nchini Libya licha ya ushauri wa serikali yao ya Misri kuwakataza wasiende huko.