Italia yawaokoa maelfu ya wahamiaji

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wahamiaji kutoka Afrika wakiwa wameokolewa na walinzi wa pwani ya Italia katika bahari ya Mediterani

Kikosi cha ulinzi wa pwani ya Italia kimesema kimewaokoa zaidi ya wahamiaji elfu mbili wakisafiri katika maboti katika bahari ya Mediterani-- katika operesheni kubwa kuliko zote kufanywa kwa wakati mmoja mpaka sasa.

Meli za jeshi la wanamaji wa Italia na meli za mizigo za kibiashara pia zilizuhiska katika operesheni hiyo.

Kikosi cha walinzi wa pwani kinasema kwa mara ya kwanza walikabiliana na watu wenye silaha wanaofanya biashara ya kusafirisha watu na kuhatarisha maisha ya wafanyakazi wake.

Wengi wa wahamiaji ambao waliondoka kutoka Libya na kujaribu kufika kisiwa cha Lampedusa -- walikuwa vijana kutoka nchi za Afrika. (wiki iliyopita zaidi ya wahamiaji mia tatu wanadhaniwa kufa baharini.).