Utafiti:Wanaume wanapenda wanawake wenye makalio makubwa

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Wanaume wanapendelea wanawake wenya makalio makubwa

Je wajua kwanini wanaume wanawapenda wanawake waliojaliwa na makalio makubwa ?

Katika majarida mengi umewaona wanaume wakikodolea macho picha za wanawake wenye makalio makubwa iwe ni kim Kardashian, Jenipher Lopez Nicki Minaj na Vera Sidika kutoka Kenya .

Sasa basi Utafiti umedhibitisha kuwa ni kweli wanaume wanapenda wanawake waliojaaliwa sehemu ya nyuma.

Kulingana na utafiti wa chuo kikuu Bilkent , chuo kikuu cha Texas, na chuo kikuu cha American University kilichoko mjini Beirut

Wanaume wanakisia kuwa mwanamke mwenye makalio makubwa anaweza kufanya kazi kwa bidii zaidi ya mwanamke ambaye hana makalio makubwa.

Hata hivyo kinachowavutia wanaume si makalio haswa bali ni kupinda kwa uti wa mgongo unaosababisha tako kuonekana zaidi.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Kim Kardashian

Utafiti huo unasema kuwa upinde wa 45.5 ndio unaovutia wanaume zaidi.

Wanaume walioneshwa picha za makalio ya wanawake wengi na asilimia kubwa iliwapendelea wanawake wenye makalio yaliyopinda kwa kiwango cha 45.5

Aidha zaidi ya asilimia 30% walisema wangalimchukua mwanamke mwenye makalio makubwa zaidi ya yule waliye naye sasa.

Kwa mujibu wa utafiti huo katika miaka ya awali mwanamke aliyeonekana kuwa na makalio makubwa alipendelewa kutokana na uwezo wake wa kubeba mizigo mgongoni.

Isitoshe mwanamke kama huyo aliwavutia wanaume wengi na hivyo kuwa na uwezo wa kuzaa watoto wengi.

Aidha mwanamke mwenye makalio makubwa angeweza kustahili uzito wa mtoto aliyebebwa tumboni na hata kustahilimi makali ya uzazi kuliko wale wenye makalio wastani.