Matumizi ya dawa katika riadha ni tatizo

Haki miliki ya picha
Image caption Lamine Diack rais wa chama cha riadha duniani, IAAF

Mwezi Desemba mwaka jana kipindi kimoja cha televisheni nchini Ujerumani kilidai kuwa maafisa wa Urusi walipokea malipo kwa mpangilio kutoka kwa wanariadha kwa kuwapatia dawa za kusisimua misuli ambazo zimepigwa marufuku michezoni na kuficha matokeo ya vipimo vya wanariadha hao.

Rais wa chama cha riadha duniani,IAAF, Lamine Diack, amesema: "ni tatizo kubwa lakini tutalimaliza kwa kusafisha lote hili."

Katika mahojiano yake ya kwanza tangu kashfa hii kutolewa hadharani,Diack amesema "alishtushwa" na "kusononeshwa" aliposikia kwa mara ya kwanza madai haya

Lakini afisa huyo mwenye umri wa miaka 81 kutoka Senegal amesisitiza kuwa tuhuma kwamba asilimia 99% ya wanariadha wa Urusi wanatumia dawa za kusisimua misuli ni "utani" na "kichekesho".

"Siwezi kukubali mtu anakuja na kusema nchini Urusi asilimia 99% ya wanariadha wanatumia dawa za kusisimua misuli. Si kweli," amesema.

"Naelewa baada ya tatizo hili watu wanasema 'Sawa, wanafanya nini, ni sahihi au hapana?', lakini nafikiri tunatakiwa kuwa wazi kwamba wanamichezo wetu asilimia 90% hadi 95% ni wasafi."Amesema rais huyo wa IAAF.