India:Uhuru wa Dini kuheshimiwa

Image caption Waandamanaji wakikemea vitendo vya mashambulizi dhidi ya Makanisa

Waziri Mkuu wa India,Narendra Modi ameahidi kulinda uhuru wa imani ya dini na kusema kuwa Serikali yake haitaruhusu kundi lolote la kidini kuwa na chuki dhidi ya jingine.

Akihutubia jamii ya kikristo mjini Delhi, ametoa wito kwa makundi yote ya kidini kuheshimiana.

Wito huo umekuja baada ya mfululizo wa matukio ya mashambulizi dhidi ya Makanisa, matukio yaliyosababisha ghadhabu miongoni mwa jamii ya Kikristo.