Rais wa Misri aomba UN kupambana na IS

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Wanamgambo wa Islamic State

Rais wa Misri,Abdel Fatah Al-Sisi ametoa wito kwa Umoja wa Mataifa kuidhinisha Operesheni ya kijeshi dhidi ya Wanamgambo wa Islamic State nchini Libya.

Rais Sisi ameiambia Redio moja kuwa Raia wa Libya wanataka hatua zichukuliwe ili kurejesha hali ya usalama na uimara katika nchi yao.

Wito wa Sisi umekuja baada ya Ndege za kivita za Misri kushambulia maficho ya IS kulipiza kisasi baada ya Raia wakristo wa madhehebu ya Coptic nchini Libya.

Siku ya jumatatu Balozi wa Misri nchini Uingereza, Nasser Kamel, alisema Boti zilizokuwa zimebeba Magaidi wanaweza kuanza kuingia barani Ulaya ikiwa hatua hazitachukuliwa.