Ngetich apigana hadi mwisho marathon

Haki miliki ya picha none
Image caption Ramani ya Kenya

Mwanariadha wa Kenya wa mbio ndefu za marathon ambaye alitambaa kufikia mstari wa mwisho amezawadiwa kutokana na ujasiri wake. Waandaji wa mbio za marathon za Austin zilizofanyika Jumapili huko Texas, Marekani walitoa zawadi ya fedha kwa Hyvon Ngetich, wakimpatia kiasi cha fedha ambacho angepata iwapo angeshika nafasi ya pili. Ngetich alikuwa akiongoza mbio hizo wakati alipoanguka mita hamsini kufikia mwisho. Akiwa amepania kumaliza mbio hizo, aliendelea kutambaa kwa mikono na magoti. Madaktari walimfuata na kiti cha kubebea wagonjwa, wakati akihangaika barabarani. Hatimaye alimaliza mshindi wa tatu.