Putin azuru Hungary licha ya maandamano

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Viongozi wazungumza kujaribu kuokoa makubaliano ya kusitisha vita

Viongozi wa Ujerumani, Urusi na Ukraine wamezungumza kwa njia ya simu, katika jitihada za kujaribu kufufua muafaka wa amani ulioporomoka kuhusu mapigano mashariki mwa Ukraine.

Pande zote husika katika mzozo huo, zilishindwa kuafikia makataa ya kuondoa silaha zake kutoka katika maeneo ya vita kufikia usiku wa manane.

Msemaji wa serikali ya Ujerumani, anasema kwamba shughuli za kuondoa silaha hizo nzito nzito zinafaa kuanza leo.

Haki miliki ya picha n
Image caption Rais Putin akiwa na waziri mkuu wa Hungary Orban

Msemaji huyo anasema wamekuabaliana kuhusu hatua muhimu ya kuruhusu wachunguzi wa kimataifa wanaofaa kufika huko ili kufuatilia kwa karibu juhudi za kuondoa silaha hizo. Aidha mazungumzo kuhusu mapigano mjini Debaltseve yamefanywa.

Kansela Angela Merkel na Rais Petro Poroshenko pia wamemsihi Rais wa Urusi Vladimir Putin kuwaamrisha wapiganaji anaowaunga mkono kukomesha mapigano.

Wakati huohuo rais Putin, anatazamiwa kushiriki mazungumzo na waziri mkuu wa Hungary Viktor Orban mjini Budapest .

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mabango yaliyobebwa na waandamanaji kumpinga rais Putin

Ziara hiyo ya Putin imewaudhi viongozi wa muungano wa NATO na wale wa umoja wa Ulaya ambao wamekuwa wakiitenga Moscow kufwatia mchango wao katika mzozo wa Ukraine.

hata hivyo bwana Orban ameshikilia kukutu kuwa taifa lake na hasa yeye mwenyewe hawezi kumtenga kamwe mfadhili wake mkuu wa gesi ya kupikia

Ziara hiyo inafanyika siku moja baada ya maandamano makubwa mjini Budapest ya kupinga ziara hiyo ya rais Putin.