Marekani na mikakati kukabili machafuko

Haki miliki ya picha AP
Image caption Maka wa Rais wa Marekani Joe Biden

Makamu wa rais wa Marekani Joe Biden amefungua mkutano wa siku tatu mjini Washington katika hali ya kupambana na kukithiri kwa machafuko.

Wawakilishi kutoka nchi zaidi ya 60 wanahudhuruia mkusanyiko huo ambao unafuatia matukio ya mauaji ya hivi karibuni katika nchi za Denmark, France na Australia pamoja na kushamiri kwa kundi la Dola ya Kiislam (IS) huko mashariki ya kati. Katika mkutano huo watajadili namna ya kupambana na misimamo mikali kama vile ushirikiano mkubwa wa masuala ya kiusalama kati ya nchi hizi. Makamu huyo wa rais amesema ilikuwa ni muhimu kushirikiana na wahamihaji ambao wanaweza kuwa na misimamo mikali kwasababu ya kuungana. Ameongeza kuwa usalama wa Taifa unaanzia katika ngazi ya jamii. Rais Barack Obama anatarajiwa kuhutubia mkutano huo