Wapiganaji 300 wa Boko Haram wauawa

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wanajeshi wa Nigeria wamesema kuwa wamewauwa zaidi ya wapiganaji 300 wa kundi la Boko Haram

Jeshi la Nigeria limesema kuwa limewauwa zaidi ya wapiganaji 300 wa Boko Haram, baada ya jeshi la nchi hiyo kutwaa tena miji kadhaa iliyotekwa na wapiganaji hao kazkazini mashariki mwa Monguno.

Msemaji wa jeshi Chris Olukolade amesema kuwa wapiganaji wachache wa kiislamu pia wamekamatwa.

Bado hakujatolewa taarifa zaidi kuthibitisha habari hizo.

Mataifa kadhaa ya magharibi mwa Afrika kama vile Niger, Chad na Cameroon, ambayo yanakabiliana na Boko Haram pia yametoa taarifa ya maafa makubwa kwa kundi hilo ambalo limeleta kero kubwa katika ukanda huo.

Siku ya jumatatu wiki hii jeshi la Nigeria lilisema kuwa limeutwaa tena mji wa Monguno, ambao ulikuwa umetekwa na wapiganaji hao wa jihadi mwezi uliopita.