Mataifa ya kiarabu yataka suluhu Libya

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Wapiganaji nchini Libya

Kundi la mataifa ya nchi za magharibi limetaka kuwepo kwa hatua za dharaua kutafuta suluhu ya kisiasa katika mzozo uliopo nchini Libya ambapo makundi hasimu yanang'ang'ania madaraka.

Taarifa hiyo kutoka marekani ,Uingereza,ufaransa,Ujerumani, Italia na Uhispania inajiri baada ya Misri kuomba msaada wa jeshi la kimataifa.

Siku ya Jumapili Misri ilithibitisha kuwa wanamgambo wa Islamic state waliwakata vichwa watu 21 raia wake ambao ni wakisristo wa madhehebu ya Copti