Umoja wa Mataifa wapinga vita Ukraine

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Moto ukiwaka katika msitu wa eneo la Debaltseve mashariki mwa Ukraine ambako waasi wanaoungwa mkono na Urusi wanadhibiti maeneo mengi.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa zimezitaka pande zinazohusika katika mgogoro mashariki mwa Ukraine kuacha mapigano na kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa wiki iliyopita ukitaka kusitishwa kwa mapigano katika eneo hilo.

Baraza la Usalama limeonyesha kusikitishwa hususan juu ya mapigano yanayotokea katika mji wa kimkakati wa Debaltseve.

Ripoti za hivi karibuni kutoka eneo hilo zinasema waasi wanaoungwa mkono na Urusi kwa sasa wanadhibiti eneo kubwa la mji huo.

Msemaji wa serikali ya Ukraine anasema mamia ya askari wa serikali walizingirwa.

Rais wa Ukraine Petro Poroshenko ameziomba nchi za magharibi kuchukua hatua kali kufuatia mapigano hayo, lakini msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani, Jen Psaki amesema mapigano hayo hayana maslahi kwa mtu yeyote kuingia katika vita na Urusi juu ya Ukraine.