Mwandishi aliyefungwa aachiliwa Burundi

Haki miliki ya picha
Image caption Waandamana Burundi wakimuunga mkono mwandishi aliyeachiliwa kwa dhamana kwa tuhuma za mauaji

Makumi ya maelfu ya raia wameandamana katika mji mkuu wa Burundi ,Bujumbura wakimuungano mkono mwandishi maarufu ambaye amewachiliwa baada ya kufungwa jela.

Walioshuhudia wanasema kuwa yalikuwa maandamano makubwa kuwahi kufanyika katika mji huo kwa miaka kadhaa.

Bobo Rugurika anayekifanyia kazi kituo cha redio cha African Public Redio aliwachiliwa kwa dhamana.

Alishtakiwa mwezi uliopita kwa kuhusishwa na mauaji ya watawa watatu raia wa Italy baada ya kurusha mahojiano hewani na mtu anayedaiwa kuwa mmoja ya wauaji.

Mahojiano hayo yalihitilafiana na uchunguzi wa polisi kuhusu uhalifu huo na kumtuhumu afisa mmoja mwandamizi.

Kituo hicho cha redio kinaonekana kupendelea upinzani.