Iraq yapanga kuwashambulia IS

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kifaru cha jeshi la Iraq

Habari za kijeshi kutoka Marekani zinasema majeshi ya Iraq na Wakurd yanapanga shambulio dhidi ya wapiganaji wa Islamic State ili kuukomboa mji wa Mosul wa pili kwa ukubwa nchini Iraq kutoka kwa wapiganaji hao.

Afisa kutoka kamndi kuu ya jeshi la Marekani amesema shambulio hilo huenda likafanyika Aprili au Mei na kwamba askari wapatao elfu ishirini na tano wote wakiwa wamefunzwa na jeshi la Marekani watatakiwa kuutwaa na kuulinda mji wa Mosul.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wapiganaji wa Islamic State

Mwandishi wa BBC mjini Washington amesema kuelezea lini shambulio litafanyika si kitu cha kawaida lakini Marekani inasisitiza kuwa wapiganaji wa Islamic State wanajipanga upya.

Wakuu wa majeshi kutoka zaidi ya nchi ishirini duniani kwa sasa wanakutana nchini Saudi Arabia kujadili njia ya kulisaidia jeshi la Iraq dhidi ya Islamic State(IS).