Samsung yakiri Tv zake zimedukua

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Samsung imekiri runinga zao zenye uwezo wa kutumia Intanet zinahitilafu

Kampuni ya kutengeza runinga ya Samsung imekiri kuwa runinga zake zimekosea kwa kutuma sauti za wateja wake bila ya kubana majina na anuani ya wateja husika.

Kosa hilo linamwezesha mtu wa tatu kubaini anuani na hata kudakua tabia za watazamaji wake wa runinga.

Hitilafu hiyo ilibainika baada ya uchunguzi uliofanywa na taasisi ya usalama wa mitandao huko Uingereza.

Samsung imesema kuwa inafanya kila iwezlo kuhakikisha wanatoa mfumo utakao bana majina na sauti ya wateja iliisijulikane wala kungamuliwa na mtu wa tatu.

"Samsung inachukulia usalama wa wateja wake kwa umakini mkubwa sana kwa hivyo tutahakikisha kuwa kuna proframu itakayofumba sauti majina na anuani ya wateja wetu," Taarifa hiyo ilisema.

"Runinga zetu za kisasa ''Smart'' zinazouzwa hivi sasa zinaprogrammu hiyo maalum na kwa zile za awali ninawahakikishia kuwa tutawatengenezea programmu yenye uwezo kama huo hivi karibuni.''

Mapungufu haya ni baadhi tu ya matatizo yaliyoikumba kampuni hiyo ambayo imekuwa ikiitengeza bidhaa za kielektroniki.

Mnamo Februari tarehe 10,Samsung ililazimika kubadili sera zake baada ya mtaalamu mmoja kubaini kuwa runing za Samsung zilikuwa zinanakili na kupeperusha taarifa za siri za wateja wake bila ya idhini yao.

Wiki iliyopita wateja wa runing zake walilalamikia mfumo ambao ulikuwa unazima runinga yao kisha inaonesha matangazo ya kibiashara.

Aidha sauti zingine za wateja zilikuwa zinatumwa kampuni ya Nuance.

Baadhi ya runinga hizo za kisasa husikiliza mambo ambayo wanasema na zinaweza kuwasilisha ujumbe kwa Samsung au mashirika yanayohusiana na Samsung kibiashara..

Onyo hilo limetolewa baada ya habari kuchapishwa katika gazeti la mtandao "Daily Beast" iliyochapisha sehemu ya sera za Samsung zinazosimamia umiliki wa kibinafsi wa televisheni zao.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Samsung imekiri runinga zao zenye uwezo wa kutumia Intanet zinahitilafu

Sera hiyo inaelezea kwamba televisheni hizo zitakuwa zinasikiliza watu katika chumba kimoja wakijaribu kutoa amri na maswali kutumia vibonyezi.

''Iwapo maneno ambayo umeyatamka ni ya kibinafsi au ya kisiri , basi ujue kuwa habari hiyo itakuwa kati ya habari zilizonaswa na kusambazwa kwa watu wengine.'' Samsung imeonya.

Kutokana na kukabiliana kuhusu taarifa ya sera yake ,Samsung imetoa taarifa kufafanua jinsi sauti hizo zinavyofanya kazi.

Inasisitiza utambuaji wa sauti unajulikana tu baada ya mmiliki kuchagua kutumia sauti badala ya kubonyeza kifaa cha kiungia mbali (remote control)

Samsung imesema kama mteja atakubali kutumia kifaa cha kugundua sauti, sauti hiyo itatambuliwa na mtu wa upande wa tatu baada ya amri ya kuitafuta sauti hiyo.

Upande watatu ambao unatafsiri sauti kutoka kwa wamiliki hufasiriwa na kampuni inayoitwa Nuance, ambayo imehitimu kutambua sauti.

Samsung si kampuni ya kwanza kujipata mashakani kwa kutumia vinasa sauti kwenye mashine na bidhaa zake.

Mwishoni mwa mwaka wa 2013,mshauri wa maswala ya kiteknolijia kutoka Uingereza aligundua kuwa televisheni yake ya LG ilikuwa inakusanya habari kuhusu tabia yake ya utazamaji wa televisheni.