Sanamu ya paka yauzwa kwa dola 80,000

Haki miliki ya picha DAVID LAY
Image caption Sanamu ya paka wa Misri yauzwa kwa dola 80,000

Sanamu moja ya paka wa Misri,ambayo nusra itupiliwe mbali kama taka,imeuzwa nchini Uingereza kwa takriban dola 80,000.

Sanamu hiyo ya shaba ,mara ya kwanza ilidhaniwa kama isio na thamani yoyote ilipogunduliwa wakati wa usafishaji wa jumba moja katika mji wa kusini magharibi wa Penzance.

Lakini baada ya kukaguliwa na wataalam ,ilibainika kuwa halisi,ikiwa ni sanamu ya miaka 2,500 kutoka Misri.