Je, sola italeta suluhu ya umeme barani Afrika?
Huwezi kusikiliza tena

Sola kuwa suluhu ya nishati Afrika

Jua huenda likawa chanzo kikubwa cha nishati duniani ifikiapo katikati ya karne hii. Tathmnini hiyo imetolewa na wachambuzi wa chama cha kimataifa cha nishati chenye makao yake mjini Paris, Ufaransa. Ripoti yao inatoa matumaini kwa takriban watu nusu bilioni barani Afrika wasio na umeme na hivyo mitambo mikubwa ya nishati ya jua ikijengwa Morocco na Kenya. Mwandishi wetu Robert Kiptoo amekwenda Turkana, kaskazini mwa Kenya, katika moja ya maeneo ya vijijini kabisa kuona kama sola inaweza kuwa suluhu.