Kufungwa kwa huduma kuathiri Wasomali

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Benki za Somalia

Ripoti mpya inasema kuwa Wasomali milioni 3 wanaotegemea kuhamisha fedha kutoka ng'ambo wako katika hatari ya kukabiliwa na njaa iwapo njia zao za kupata fedha zitafungwa.

Onyo hilo linajiri wiki mbili tu baada benki ya Marekani Merchants Bank of California ambayo imekuwa ikishughulikia uhamishaji wa fedha kwa 80% kutoka Marekani hadi Somalia kufunga huduma zake kutokana na wasiwasi kuwa fedha hizo zilikuwa zinawafikia wapiganaji wa Al-Shabaab.

Mwaka uliopita Benki ya Barclays nchini Uingereza ilifunga huduma ya kusafirisha pesa katika akaunti za Somali na benki za Australia vile vile zinafikiria kuchukua hatua ama hiyo.