Ulaya kuridhia kuinusuru Ugiriki?

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Waziri wa Ugiriki,Yanis Varoufakis

Serikali ya Ugiriki inatarajiwa hii leo kuuomba rasmi Umoja wa Ulaya kuongezewa muda wa miezi sita kudhaminiwa, huku ikikwepa kuridhia kuchukua hatua za kubana matumizi.

Ugiriki ina matuamaini ya kuwasilisha ombu hilo ambalo ina matuamaini ya kuweza kukidhi matakwa ua ukanda wa Ulaya kwa ajili ya mabadiliko ya kiuchumi.

Ujerumani inasisitiza sana dhamana ikimaanisha kuwa sharti la kubana matumizi liko palepale.Bila hilo Ujerumani inasema hakuna makubaliano yeyote itakayoingia.

Ugiriki iko hatarini kufilisika ifikapo mwishoni mwa Mwezi wa pili, isipokuwa tu ombi la Ugiriki litakapokubaliwa.

Benki kuu ya Ulaya imekubali kuto fungu la nyongeza kwa Benki za Ugiriki kama dharula.

Kiasi cha msaada wa pesa kilichotolewa kwa dharula kwa ajili ya Benki za biashara nchini humo zilifikia dola bilioni 77.