Kwa nini mapigano hayakomi Ukraine?

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mapigano yameendelea mjini Debaltseve

Ofisi ya Rais nchini Ufaransa imesema Viongozi wa Urusi,Ukraine, Ufaransa na Ujerumani wamekemea ukiukwaji wa makubaliano ya kusitisha mapigano Mashariki mwa Ukraine .

Baada ya Mazungumzo ya simu kati ya Viongozi wanne wa Nchi hizo,walitoa wito wa utekelezwaji wa makubaliano yaliyowekwa mjini Minsk juma lililopita, ikiwemo kuacha kabisa mapigano.

Waangalizi wa kimataifa wanaofuatilia utekelezaji wa makubaliano hayo nchini Ukraine wamesema pande zote mbili zinajutia kushindwa kutekeleza makubaliano mjini Debaltseve.

Imeripotiwa kuwa maeneo mengine mapigano yamekoma