WHO:Magonjwa ya Kitropiki hatari zaidi

Image caption Ugonjwa wa Matende husababisha ulemavu

Shirika la Afya duniani, WHO limeanzisha Kampeni ya kutoa uelewa kuhusu maradhi 17 yanayoathiri ukanda wa tropiki ambayo yanaathiri Watu bilioni moja na nusu duniani.

WHO imezitaka Serikali duniani kuwekeza katika mapambano dhidi ya Maradhi ya kitropiki yanayoelezwa kupuuzwa, kama vile Malale na Matende ambao husabisha ulemavu na vifo katika nchini zinazoendelea.

Mwandishi wa Ripoti hiyo, Dokta Dirk Engles ameiambia BBC kuwa magonjwa mengi yangeweza kudhibitiwa kwa matibabu lakini ni wazi kuwa magonjwa mengine yanayoonekana yamechukua nafasi kubwa katika kushughulikiwa kwa haraka kama vile Ebola.