Huwezi kusikiliza tena

Congo yalaumiwa kutolinda Watoto

Nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, watoto wenye umri chini ya miaka kumi na nane wamekuwa wakifanyishwa kazi migodini. ili kuwawezesha kukidhi mahitaji yao pamoja na familia kutokana na umaskini.

Mashirika ya kutetea haki za watoto yanailaumu serekali ya nchi hio kwa kutochukua hatua madhubuti dhidi ya Kampuni za uchimbaji madini zinazoajiri watoto.

Mwandishi wetu wa mashariki mwa Kongo BYOBE MALENGA ametembelea kijiji cha Kamituga magharibi mwa mji wa Bukavu katika jimbo hilo.