Serikali yakubaliana na waasi Mali

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Wapiganaji waasi wa MNLA

Serikali ya Mali imekubali kusitisha uhasama na Waasi wa Tuareg kaskazini mwa Nchi hiyo.

Makundi yaliyotia saini makubaliano ya kusitisha mapigano nchini Algeria.Makundi yaliyotia saini makubaliano nchini Algeria ni pamoja na Tuareg,MNLA na Waasi wa Kiarabu Azawad au MAA.

Makubaliano hayo ni sehemu ya mazungumzo yanayoendelea ya kurejesha hali ya utulivu kaskazini mwa Mali, miaka miwili baada ya Jeshi la Ufaransa kuwafurusha Waasi wa kiislamu.

Lakini kumekuwa na wasiwasi kuwa bado itakuwa vigumu kupata suluhu hasa kwa mambo kama ya kukabidhi Madaraka kaskazini mwa Mali ambapo Waasi wanaita Azawad.