Oxfam:Watu 50,000 wametoroka Darfur

Haki miliki ya picha .
Image caption Baadhi ya watoto ambao wazazi wao wamelitoroka eneo la Darfur

Shirika la wahisani la Oxfam limesema kuwa zaidi ya watu elfu hamsini kutoka eneo la Darfur huko Sudan wamekimbia makazi yao tangu mwaka uanze.

Linasema watu wanaokimbia mapigano yaliyozuka upya wanaishi katika maeneo ya wazi na wanaobahatika wanakaa chini ya miti.

Baadhi ya familia zilipoteza watoto wake njiani.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Baadhi ya wanawake katika eneo la Darfur.zaidi ya watu 50,000 waleitoroka eneo hilo mwaka huu pekee

Chakula, mifugo na mali nyingine imeporwa vijijini.

Mzozo huo wa Darfur umekuwa ukiendelea kwa karibu miaka kumi na miwili.

Kumekuwa na mikataba mingi ya amani kati ya serikali na makundi mbalimbali ya waasi lakini imekuwa ikiporomoka baada ya kutiwa saini.