Mugabe atimia miaka 91

Rais Robert na Grace Mugabe Haki miliki ya picha bbc

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe ametimia miaka 91 Jumamosi.

Yeye sasa ni kiongozi mzee kabisa duniani na amekuwa madarakani kwa miaka 35.

Sherehe ya siku yake ya kuzaliwa itafanywa baada ya juma moja.

Anatarajiwa kufanya pati kubwa katika uwanja wa golf huko Victoria Falls - inakisiwa pati itagharimu dola milioni moja.

Maelfu ya watu watahudhuria karamu hiyo ambapo kutachinjwa ndovu, nyati, paa na simba mmoja.

Shirika la habari la taifa linasema wananchi watalipia pati hiyo.

Zimbabwe ni moja kati ya nchi maskini duniani.