Robert Mugabe afikisha miaka 91

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe ametimia miaka 91 leo.

Yeye sasa ni kiongozi mzee kabisa duniani, na amekuwa madarakani kwa miaka 35.

Sherehe ya siku yake ya kuzaliwa itafanywa juma lijalo.

Anatarajiwa kufanya sherehe kubwa katika uwanja wa golf huko Victoria Falls, inakisiwa sherehe yenyewe itagharimu dola milioni moja.

Haki miliki ya picha APTN
Image caption Rais Mugabe aanguka katika mkutano wa mataifa ya Afrika mjini Addis Ababa Ethiopia

Maelfu ya watu watahudhuria karamu hiyo, ambapo kutachinjwa ndovu, nyati, paa na simba mmoja.

Shirika la habari la taifa linasema wananchi watalipia dhifa hiyo

Zimbabwe ni moja kati ya nchi maskini duniani.