Watoto wengi watekwa Sudan Kusini

Vijana wadogo  katika vita vya Sudan Kusini

Umoja wa mataifa unasema kuwa vijana kadha, wengine wa umri wa miaka 13 tu, wametekwa nyara Sudan Kusini.

UNICEF inaeleza kuwa kama 89 walitekwa na wanaume waliokuwa na silaha ambao walipita majumbani kutafuta watoto wa kiume wa zaidi ya miaka 12.

Baadhi yao walinyakuliwa wakati wanafanya mitihani.

Mambo hayo yalitokea kwenye kambi katika jimbo la kaskazini la Malakal, ambalo lina maelfu ya watu waliokimbia vita baina ya wanajeshi wa serikali na wapiganaji.

Pande zote mbili katika vita hivyo wametuhumiwa kuwa wanatumia watoto vitani.