Al Shabaab yatishia kushambulia Ulaya

Westgate Nairobi baada ya shambulio la Al Shabaab  2013 Haki miliki ya picha Kenyan Presidential Press Service Getty

Waziri wa Usalama wa Marekani anasema analitia maanani sana tishio la kundi la Waislamu wa Somalia, Al Shabaab, kwamba litashambulia maeneo ya maduka huko Marekani, Canada na Uingereza.

Katika mahojiano kwenye televisheni, Jeh Johnson alisema pametokea mabadiliko katika vitisho vya makundi ya wapiganaji Waislamu ambayo sasa yanatoa wito kwa washabiki wao katika nchi maalumu kufanya mashambulio.

Ulinzi umezidishwa kwenye eneo moja la maduka la Marekani katika jimbo la Minnesota, ambalo lina wakaazi wengi Wasomali

Mwaka wa 2013, shambulio lilofanywa na Al Shabaab dhidi ya eneo la maduka la Westgate mjini Nairobi, Kenya, liliuwa watu zaidi ya 60.