Mourinho alalama kuhusu sare na Burnley

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mkufunzi wa Chelsea Jose Mourinho

Mkufunzi wa kilabu ya Chelsea Jose Mourinho amelaumu visa vinne vilivyosababisha kilabu yake kushindwa kuifunga Burnley.

Mchezaji wa The Blues Nemanja Matic alionyeshwa kadi nyekundu huku Chelsea ikilazimika kupata sare ya 1-1 nyumbani darajani.

Akifuatilia daftari yake,baada ya mechi hiyo kukamilika wakati wa mahojiano na BBC,Mournho alisema:

''Kuna visa vitatu katika mechi hii ambavyo unaweza kufanya stori.Dakika ya 30,33,43 na 69.Usiniulize maswali mengi;Siwezi kukufahamisha tena kuhusu visa hivyo.Mimi huadhibiwa wakati ninapovitaja''.