Miaka 2 jela kwa kuigiza ufalme Thailand

Haki miliki ya picha AP
Image caption Patiwat Saraiyaem aliyehukumiwa kifungo kwa kuukejeli Ufalme wa Thailand

Mahakama nchini Thailand imewahukumu wanafunzi wawili kifungo cha miaka miwili na nusu jela kila mmoja kwa kucheza mchezo uliotajwa kuwa uliuchafulia sifa ufalme .

Pornthip Munkhong na Patiwat Saraiyaem ni miongoni mwa wanafunzi walioandaa mchezo wa kuigiza ulioitwa mke wa mbwa mwitu Fisi yaani wolf's bride, katika chuo moja kikuu mjini Bangkok mwaka wa 2013.

Mchezo huo uliotumiwa kusherehekea ushindi wa wanafunzi wa kupinga utawala wa kijeshi miaka 40 iliyopita na haukuwa na ushawishi mkubwa nje ya chuo kikuu.

Lakini baada ya mapinduzi ya kijeshi mwaka uliopita, wakuu wa jeshi walishinikiza hatua za kisheria kuchukuliwa dhidi ya mtu yeyote au kundi lolote ambalo linakejeli ya kutusi utawala wa kifalme nchini humo, na hapo ndipo

wanafunzi hao walipokamatwa.

Wawili hao walikiri mashtaka dhidi yao ili kupata huruma ya kushawishi mahakama hiyo kupunguza hukumu yao,kwa kuwa ni vigumu sana kwa washtakiwa kushinda kesi kama hiyo na mara nyingi adhabu yake huwa kifungo cha

kati ya miaka kumi na ishirini gerezani.

Wanafunzi hao wanaamini kuwa wao hawakuwa na kosa lolote.

Mchezo huo uliangazia mfalme mmoja wa kudhaniwa aliyekuwa na chongo sawa na ya mfalme Bhumibol Adulyadej,ambaye alipoteza jicho lake moja akiwa mchanga, na kwa kufananisha hilo wakajiweka katika hatari ya

kufunguliwa mashtaka.

Jaji aliyesikiliza kesi hiyo alisema kuwa anafahamu kuwa washtakiwa walikuwa vijana wenye umri mdogo lakini walikuwa wamedunisha hadhi ya ufalme wa nchi hiyo, kitendo ambacho kwa mujibu wa sheria za nchi hiyo adhabu

yake huwa kifungo gerezani.