Amnesty imetaka kura ya turufu isitumike

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wanamgambo wa Islamic State

Shirika la haki za binadamu la Amnesty International lenye makao yake makuu huko Washington Marekani, limewataka wanachama wa kudumu wa baraza la usalama la umoja wa mataifa kutotumua kura yao ya

turufu wakati maafa yanapotokea.

Katika ripoti yake ya kila mwaka Amnesty International limesema kuwa mwaka wa 2014 ulikuwa ni mwaka ambao mamilioni ya watu walijikutaka kwenye matatizo makubwa zaidi lakini limesema kuwa hatua za kimataifa dhidi ya

hilo zilikuwa za kufedhehesha.

Shirika hilo limesema kuwa mara kadhaa wamekuwa wakiweka maslahi ya nchi mbele kuliko maswala ya haki za binaadam.

Amnesty International imesema viongozi wa dunia walitakiwa kuchukua hatua mapema kushughulikia migogoro ambayo imewaacha Watu zaidi kulazimika kuishi chini ya udhibiti wa Makundi ya kigaidi kama vile Islamic State.