Ngoma na vuvuzela zaipiku simu Malawi

Image caption Nchini Malawi vuvuzela inaaminika zaidi kuliko simu.

Jamii nchini Malawi wanapendelea zaidi kuwasiliana kwa njia za asili zaidi ya kuliko ambavyo karne hii ya sayansi na teknolojia inavyofanya,hivyo jamii hizo hutumia zaidi ngoma za asili,ama vuvuzela kama njia ya mawasiliano na wamezipa kisogo simu za kisasa ama radio pale ambapo jamii yao ikikumbwa na janga lolote, basi njia za asili ndio mwafaka kwao.

Kwa kawaida sisi hutumia njia hizi za asili kwasababu simu za kisasa haziaminiki,asema bwana Ndamiwe Kalambo,na pia amewataka viongozi wa kiserikali pamoja na wananchi wajadili kwa kina juu ya masuala ya majanga ya asili pindi yatakapo watokea kama mafuriko ni hatua gani ambazo watapaswa kuzichukua na kufikisha taarifa kwa wakati.

Akitetea hoja ya utumizi njia za asili zaidi Ndamiwe anasema kwamba maeneo mengi ya nchi hiyo hayana mawasiliano ya uhakika na hata mtandao haukamati asilani,na hivyo hata ujumbe wa dharura utumwapo haufiki kwa wakati kwa wahusika na hivyo mawasiliano ya kisasa si rahisi hivyo.

Image caption Chombo hiki malawi sio ssaaaana kiviiile.

Taarifa zinaeleza kwamba jamii ya Kilupula ilikumbwa na mafuriko,kulikuwa na mkutano wanakijiji walikuwa wakipiga mayowe ya kuomba msaada,wengine walikuwa wakipiga ngoma,wengine walikuwa wakipuliza filimbi ama vuvuzela ili kupeleka ujumbe wa dharula ama mwito wa kuomba msaada.

Kalambo aliwaambia viongozi wa kiserikali kuwa ,ujumbe wa serikali wa dharula ama kuomba msaada unapaswa kusambazwa kwa jamii nzima ya Malawi kwa ujumbe mfupi sawa na wakati wa upigaji kura ili kuongeza nafasi ya ujumbe mfupi kuwafikia walengwa kwa wakati.

Tangu mwaka 1984,Malawi imeshakumbwa na mafuriko mara ishirini na tisa,imepigwa na vimbunga mara tatu na imeshakumbwa na ukame mara saba, na njia ya mawasiliano wanayoitumia zaidi ni ya asili na vuvuzela linaongoza kwa matumizi.

Wengine wanalitumia vuvuzela michezoni lakini Malawi wanalitumia kama njia ya mawasiliano.