Waislamu wanazidi kubaguliwa UK

Image caption Waislamu nchini Uingereza wamepinga ghasia dhidi ya gazeti la Charlie hebdo

Idadi kubwa ya waislamu nchini Uingereza wanapinga ghasia dhidi ya watu waliochapisha vibonzo vya kumdhalilisha mtu Mohammed,uchunguzi uliofanywa na BBC umebaini.

Utafiti huo vilevile umebaini kwamba wengi hawana huruma na wale wanaopigana na maslahi ya mataifa ya Magharibi.

Image caption Uchunguzi umebaini kuwa Waislamu wengi wanabaguliwa nchini Uingereza

Lakini asilimia 27 ya waislamu 1000 waliohojiwa na ComRes wanasema waliunga mkono sababu za shambulizi hilo la mjini Paris.

Image caption Waislamu wakiwa katika Ibada Uingereza

Karibia asilimia 80 wanasema kuwa walikerwa wakati picha zinazomdhalilisha mtume zilipochapishwa.

Image caption Uchunguzi umebaini kuwa Waislamu wengi wanabaguliwa nchini Uingereza

Zaidi ya asilimia 68 waliohojiwa walisema kuwa ghasia dhidi ya wale waliochapisha vibonzo hivyo hazikuwa za haki.

Image caption Waislamu nchini Uingereza

Lakini utafiti huo uliofanywa kati ya January 26 na Februari 20,unasema kuwa asilimia 32 ya waislamu nchini Uingereza hawakushangazwa na shambulizi la gazeti la Cherlie Hebdo ambalo lilichapisha vibonzo vya

mtume pamoja na eneo la kuuzwa vyakula vyenye mahitaji ya wayahudi mjini Paris.