Mtandao wa 5G? Subiri hadi mwaka wa 2020

Haki miliki ya picha Thinkstock
Image caption Wanasayansi wamefaulu kuzindua mtandao wa 5G

Wanasayansi wanaofanya majaribio ya kasi ya mtandao wa simu za kisasa 5G wakitumia kasi ya intanet wanasema kuwa wamesajili kasi ya juu zaidi katika mfumo ujao wa 5G.

Watafiti hao kutoka kitengo cha ubunifu kutoka chuo kikuu cha Surrey Uingereza , ''5G Innovation Centre'' wanasema kuwa walifaulu kusajili terabit moja kwa sekunde (Tbps) ambayo ni maradufu ikilinganishwa na mfumo unaotumika sasa wa

4G katika mataifa mengi yanayostawi.

Teknolojia hiyo mpya inaratibiwa kufanyiwa majaribio ya uma ifikapo mwaka wa 2018.

Aidha watafiti wa sekta hiyo ya mawasiliano Ofcom wanakisia huenda Uingereza ikashuhudia mtandao unatumia kasi hiyo ya 5G mwaka wa 2020.

Ilikubaini kasi wanayozungumzia,watafiti hawa wanadai kuwa itakuwarahisi sana kutoa mtandaoni filamu ya saa nzima kwa sekunde 3 pekee.

Haki miliki ya picha Thinkstock
Image caption Mashirika makubwa ya simu yameungana na serikali kufadhili utafiti kuhusiana na mtandao wa masafa ya 5G

5G wanasema inayotumia kasi ya 1Tbps, ni bora mara 65,000 zaidi ya mtandao bora kwa sasa wa 3G na 4G.

Changamoto wanayoikabiliwa nayo hata hivyo ni kufanya majaribio wakitumia simu za kisasa (Smartphones)

Kulingana na Prof Tafazolli anayeongoza utafiti huo jopo la wanasayansi litaendelea na majaribio katika ardhi ya chuo hicho kikuu kabla ya kufanya majaribio nje.

Mfumo huo wa 5G unapaswa kupigwa msasa kikamilifu wakitumia uwezo wa gigahertz 6GHz.

''hatujui iwapo mtandao huu utakuwa wazi kwa umma mwaka wa 2020, 2030 ama 2040 unachokijua ni kuwa kufikia wakati huo sharti kuwe na muundo msingi wa kupokea masafa ya kasi kama hii'' alisema Prof Tafazolli .