Ajitolea kutoa ubikira siku ya wanawake

Image caption Mwanamume aliyejitolea kuuza ubikira wake wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani

Mwanamume mmoja amejitolea kutoa ubikira wake wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya wanawake.

Sorin Gorgian Salinievcici mwenye umri wa miaka 24 amejitolea kuuza ubikira wake kwa pauni 1,476 baada ya kusoma kuhusu wanawake wanaofanya hivyo.

Alielezea kuwa :''mimi husoma kuhusu wasichana wanaofanya hivyo na nikafikiri kwamba iwapo wanafanya hivyo hata mimi naweza kufanya''.

Amesema kuwa mwanamke yeyote atakayenunua ubikira wake ni sharti awe mwenye heshima.

''Sisemi kuwa ni lazima awe mrembo lakini awe mwanamke wa kawaida, mzuri na mwaminifu''.alisema.

Katika bango aliloandika nyumbani kwake huko Romania,alisema kuwa inaweza kuwa zawadi nzuri katika maadhimisho ya siku hiyo ya wanawake mnamo mwezi machi tarehe 8.

Je,unadhani kitendo hiki kinakubalika?