Nyong'o aibiwa vazi lake la bei Mbaya

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Lupita Nyong'o akiwa amevalia vazi linalotajwa kuwa na gharama kubwa

Nguo iliyobuniwa na kampuni ya Calvin Klein yenye thamani ya dola 150,000, na kuvaliwa na msanii maarufu wa kike Lupita Nyong'o katika tuzo za Oscar imeibiwa Hollywood .

Gauni hilo lililobuniwa kwa namna ya pekee na kupambwa kiasilia na konokono weupe zaidi ya 6,000 toka baharini, lilichukuliwa kwenye hoteliya London magharibi mwa Hollywood.

Lupita Nyong'o kutoka nchini Kenya aliibuka msanii bora wa kike mwaka jana baada ya miaka kumi na mbili ya utumwa, Lupita alikuwa mtangazaji wa sherehe za jumapili.

Baadhi ya magazeti yanamwita Lupita Nyong'o mrembo wa mwaka 2014.

Sheriff William Nash anasema nguo hiyo inaonekana kuibiwa siku ya jumatano jioni na polisi wanaendelea kufanya uchunguzi kupitia kamera maalum za CCTV.