Serikali yahusishwa na watekaji S Kusini

Haki miliki ya picha UNICEF
Image caption UN inasema kuwa kundi la wapiganaji waliowateka vijana nchini Sudan kusni linahusishwa na serikali

Umoja wa mataifa unasema kuwa vijana wa kiume waliotekwa juzi nchini Sudan Kusini huenda walichukuliwia na kundi la wapiganaji lenye uhusiano na serikali.

Shirika la watoto la umoja wa mataifa UNICEF linasema kuwa idadi ya watoto waliotekwa na kundi la Shilluk walikuwa mamia na sio 89 jinsi ilivyoripotiwa awali.

Walioshuhudia walisema kuwa wengi wa watoto hao wamepelekwa kwenye kambi ya mafunzo kwenye jimbo la Upper Nile na watoto walio hadi chini ya miaka 12 walikuwa wakibeba bunduki.