Mfungwa wa kisasa atoroka jela Burundi

Image caption Aliyekuwa mwenyekiti wa chama tawala nchini Burundi Hussein Rajabu ameripotiwa kutoroka jela.

Aliyekuwa mwenyekiti wa chama tawala nchini Burundi Hussein Rajabu ameripotiwa kutoroka jela.

Hussein Rajabu ambaye alikuwa mwanasiasa mashuhuri nchini humo alihukumiwa kifungo cha miaka 13 jela, mwaka 2007.

Bwana Rajabu alishitakiwa kwa kutaka kuzusha vurugu nchini.

Haijabainika ni kwa jinsi gani alifanikiwa kutoroka.

Alikuwa akitumikia kifungo cha miaka 13 kwa kupanga kuipindua serikali .

Kabla akamatwe mwaka 2007 Hussein Radjabu alikuwa mshirika wa karibu wa rais wa Burundi Pierre Nkurunziza na mwenyekiti wa chama tawala.