Biashara ya Hina yashamiri Zanzibar

Image caption Siku hizi hina ya kuchora kwenye vitambaa ndiyo inayolipa.

Kwa miongo kadhaa Wanawake wa Tanzania waishio Visiwani Zanzibar,wamekuwa wakijiremba mikono na miguu yao kwa hina. Wanapopaka hina mwilini, baada ya muda fulani hufifia lakini kundi moja la wanawake wamegundua namna ya kuhifadhi na kudumisha utamaduni huo kwa njia ya kisasa.

Akikaa chini ya kivuli cha mti,kwenye mkeka,msanii Mashavu Salum yuko makini katika kumhudumia mteja akitumia kijiti kidogo kuchotea tope la hina kwenye kifuniko cha chupa na kumchora mteja wake pole pole kwenye mguu. Sanaa hii inahusisha ubunifu wa kuchora, urembo wa maua na michoro mingine yenye nakshi .

Hina ilitoka India na kuletwa huku na mababu zetu…Sana sana kama kuna harusi anayepakwa hina ni bibi harusi anayeolewa au kuna sikukuu, watoto wanapopakwa hina ni kama kitu cha furaha.Lakini kama una matatizo uma a shida, haikujii hamu ya kuchora hina.”

Miaka ya karibuni, imewapa wasanii faida na kuwavutia wageni wanotembelea kisiwa hicho hasa wanawake kupata muonjo wa utamaduni huo wa furuha.

Inapopakwa mwilini ,nakshi za hina hufufia kutoka kwenye ngozi baada ya muda wa wiki moja au mbili.Lakini kundi la wanawake Zanzibar wanahakikisha Hina inakaa muda mrefu

“Mwanzo tulipo toa hina kwenye mwili kuitia kwenye canvas,of course jambo la mwanzo lazima tulipata shida kidogo kwa sababu hujazoea,kutumia rangi.Lakini baadaye, baada ya muda ya miezi sita,tulikuwa wazoefu sana tulikuwa na furaha sana.”

Kwa kutumia rangi za acrylic hutokezea Zaidi na kuonyesha baadhi ya mitindo ya mauamaua. michoro hiyo na ishara tofauti hutegemea hisia za msanii.

Msaada kutoka wafadhili wa ki Marekani huwafundisha ujuzi wa kuchora kwenye maturubai imewaruhusu kuongeza vipato vyao.

CANVAS

Image caption Biashara ya Hina vitambaani ndiyo inayolipa

“Kwenye mwili unaweza ukachora mara kwa mara lakini pesa inakuwa ndogo sana lakini,kwenye kanvas unauza!Kwenye mwili unaweza ukamchora mtu elfu kumi au elfu ishirini,lakini kwenye kanvas unaweza ukauza hata kwa dola 200.”

Hadi sasa Wanawake hao wameweza kuonyesha ubunifu wao nchini Tanzania na nje ya mipaka,katika nchi za Marekani,Canada na China, wakiwa na matumaini ya kukuza zaidi sanaa hii siku za usoni.