China yaongeza bajeti yake ya Jeshi

Haki miliki ya picha REUTERS
Image caption Wanajeshi wa China

China inasema kuwa bajeti yake ya ulinzi itaongezeka kwa asilimia kumi mwaka huu.

Wanajeshi wake wanatarajiwa kupewa dola bilioni 145 na kuendelea na mfumo wa kuongeza bajeti ya jeshi ulioanza miaka 20 iliyopita.

Taifa la Marekani ndilo hutumia fedha nyingi zaidi kwa bajeti ya jeshi.

Akitoa tangazo hilo msemaji wa serikali Fu Ying alisema kuwa China imejifunza kutokana na historia.

Japan nayo iliongeza bajeti ya jeshi lake mwaka huu baada ya kuipunguza kwa miaka mitatu mfululizo.