Wanawake wa Algeria walindwa na sheria

Image caption Mwanamke wa Algeria

Bunge nchini Algeria limepitisha sheria hivi leo inayo eleza kuwa unyanyasaji wanawake nchini humo ni kosa la jinai ,hatua ambayo imepingwa vikali na makundi mawili, la watunga sharia na pia Amnesty.

Sheria hiyo inaelekeza kuwa manyanyaso yatakayo tendwa yatasababisha maumivu ama madhara ya mwili adhabu iliyopendekezwa ni kifungo cha miaka ishirini jela,na sheria pia inamruhusu jaji kutoa adhabu ya kifungo cha maisha jela kwa makosa ya unyanyasaji majumbani ambao umesababisha kifo.

Muswada huo umepita kwa kura ya nusu ya wabunge wa bunge la nchi hiyo waliohudhuria kikao cha bunge wapatao 462,matokeo hayo yanaibua hasira ya baadhi ya wabunge wenye kushikilia msimamo mkali wa dini ya kiislam.

Abdelallah Djaballah wa chama cha El Adala anasema kwamba sheria hiyo mpya inalipa kisasi kwa waume na wanaume kwa ujumla wa chi hiyo na kuwalaumu watunga sheria kwa kuthubutu kutaka kuzisambaratisha familia.

Kutokana na hayo kwa upande mwingine chama tawala nchini Algeria waao wameiita siku ya leo kuwa ni siku kubwa kwao kwa kuchukuliwa hatua za kukomesha ukatili dhidi ya wanawake.

Kila mwaka inakadiriwa wanawake kati ya 100 hadi 200 hufa kila mwaka nchini humo kwa unyanyasaji wa majumbani hii ni kulingana na takwimu zilizochapishwa na vyombo vya habari.

Amnesty International imetaka kufanyike marekebisho ya shetia hiyo ili kuondoa kipengele kinacho mtaka manusura wa manyanyaso hayo kuwataka radhi wahusika na kuita kipengele hicho kuwa ni cha hatari ya kihistoria .

Kushindwa kukiondoa kingele hicho,kutasababisha kuwaanika hadharani wanawake watakao kuwa wakieleza unyanyasaji wa majumbani waliotendewa kwenye hatari kubwa ya kufanyiwa vurugu na utumizi wa nguvu kuwalazamisha kufuta madai yao.