Ford yazindua baiskeli ya kielektroniki

Haki miliki ya picha Ford
Image caption baiskeli inayotumia umeme

Kampuni ya kutengeza magari ya Ford imezindua baiskeli ya kielektroniki kwenye mkutano mkubwa wa magari duniani katika mpango wake wa upanuzi.

Kampuni zaidi za kutengeza magari zinatafuta njia mbadala za kutengeza pesa huku nyingi zikitengeza kile kinachoitwa kama uchukuzi wa haraka.

Baiskeli hizo zinazotumia umeme ziko aina mbili,moja inayotumiwa na wasafiri na nyengine inayotumiwa kufanya biashara.

Baiskeli zote mbili zina programu za smartphone zinazoweza kumuelekeza anayeziendesha.

Jaribio la baiskeli hizo ni miongoni mwa mipango ya kampuni ya Ford kubuni mbinu mpya ya usafiri huku ikifanya utafiti kuhusu vile baiskeli hizo zinzovyoweza kuingiliana na magari pamoja na usafiri wa uma.

''Kuna mbinu nyingi za kuzunguka mjini.Lakini kile kinachohitajika ni njia za kuunganisha mbinu hizi zote za usafiri pamoja amesema Ken Washington'',makamu wa rais wa kitengo cha utafiti cha Ford .