Palestina yakomesha ushirikiano na Israeli

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Ushirikiano wakiusalama ulianza 1993

Mamlaka ya kipalestina Palestine Liberation Organisation imekomesha ushirika wake wa usalama na Israel.

Ushirikiano huo ulikuwa sehemu ya makubaliano ya Oslo mwaka wa 1993.

PLO imesema kamati yake kuu itakutana kutekeleza uamuzi huo uliochukuliwa katika mkutano wa baraza kuu katika mji wa Westbank Ramallah.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mamlaka ya kipalestina Palestine Liberation Organisation imekomesha ushirika wake wa usalama na Israel.

Tangazo hilo linachukuliwa kama kisasi kwa Israel kwa kukata uhamishaji wa ushuru kianzo cha fedha kwa utawala wa Palestina .

Mwandishi wa BBC aliyeko Jerusalem anasema kuwa mwandishi wa BBC huko Jerusalem anasema kuwa ikiwa ushirikiano huo utamalizika itakuwa pigo kwa usalama wa Israel na inatarajiwa kujibu vikali.

Kauli hiyo ya Palestine Liberation Organisation (PLO) inamaanisha kuwa Wapalestina hawatatoa habari tena kuhusu makundi yenye waislamu wenye siasa kali kama vile Hamas.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Hii inamaanisha kuwa ujasusi dhidi ya makundi ya waislamu wenye msimamo mkali haitakuwepo tena

Israel ilisimamisha mpango wa kutuma kodi kwa mamlaka ya Kipalestina baada ya Wapalestina kutuma ombi la kutaka kujiunga na mahakama ya jinai duniani ICC yenye makao yake hague Uholanzi mwezi januari.

Kutotumwa kwa kodi hiyo ambayo huchangia pakubwa kwa pato la taifa kumewapelekea wafanyikazi wa sekta ya uma katika eneo la Palestina kukosa mishahara

Israeli haijatoa taarifa yeyote kufuatia kauli hiyo ya mamlaka ya kipalestina